Home Uncategorized JONAS MKUDE RUKSA KUSEPA SIMBA, TP MAZEMBE WAITWA MEZANI

JONAS MKUDE RUKSA KUSEPA SIMBA, TP MAZEMBE WAITWA MEZANI

JONAS Mkude, kiungo mkabaji ndani ya Klabu ya Simba ni miongoni mwa wazawa wenye vipaji ambao kwa sasa inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya Klabu ya TP Mazembe.

Sababu kubwa za TP Mazembe ya Congo kuanza kumfuatilia nyota huyo ni uwezo wake makini ambao haujawahi kuchuja kila anapopata nafasi ndani ya uwanja. 
Uongozi wa Simba umebariki ishu yake ya kuibukia Congo iwapo utaratibu utafuatwa kwa kuwa wanaamini kuwa mpira ni biashara.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa:”Hakuna mtu anaweza kumzuia mchezaji kuondoka ndani ya timu kwa sasa, mpira ni biashara hivyo kama hao watu wa Congo wanataka saini kama ambavyo inaelezwa basi waje mezani.” Msimu huu wa 2019/20 Mkude amehusika kwenye mabao manne ya Simba kati ya 63.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA