Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUPOTEZA MCHEZO WA KWANZA,GAMONDI ASEMA HAYA KUELEKEA MCHEZO WA...

BAADA YA YANGA KUPOTEZA MCHEZO WA KWANZA,GAMONDI ASEMA HAYA KUELEKEA MCHEZO WA KESHO

Habari za Yanga leo

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema makosa waliyoyafanya dhidi ya CR Beloizdad hawatayarudia katika mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly.

Yanga wanashuka dimbani kesho Desemba 2,2023 kucheza na Al Ahly ukiwa ni mchezo wao wa pili baada ya kupoteza wa awali dhidi ya CR Beloizdad kwa magoli 3-0.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo muhimu kwa Yanga kwa ajili ya kufufua matumaini yao katika mashindano hayo makubwa Afrika, Gamondi amesema hawataruhusu makosa waliyofanya dhidi ya CR Beloizdad.

“Tunafahamu tunacheza na klabu kubwa Afrika, hatutaruhusu makosa kama yale tuliyofanya kwenye mchezo wetu uliopita, hizi timu kubwa ukifanya makosa kidogo tu unaadhibiwa tofauti na kwenye ligi ya ndani, unaweza kufanya makosa na usiadhibiwe,” alisema Gamondi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTAMBA MISIMU MIWILI LIGI KUU..HIVI NDIVYO BIASHARA UTD INAVYOENDA KUFA...WACHEZAJI WAIKIMBIA...