Home Habari za michezo ZA NDAAANI KABISA…MASTAA YANGA WALIA HALI NGUMU…HAWAJALIPWA MSHAHARA…

ZA NDAAANI KABISA…MASTAA YANGA WALIA HALI NGUMU…HAWAJALIPWA MSHAHARA…

Habari za Yanga

Wachezaji wa Yanga Princess wamedaiwa kugoma kuondoka makwao wakishinikiza kulipwa fedha zao za usajili na mishahara.

Ligi ya Wanawake imemalizika tangu Mei 17 2023, lakini mpaka leo wachezaji hawajavunja kambi kitu ambacho si kawaida wachezaji kubaki kambini ilhali hakuna mashindano.

Wale wachezaji wa kigeni wamekatiwa tiketi za kuondoka tarehe 8 ya mwezi huu wa 6 hali iliyozua taharuki kwa nini wakatiwe tiketi za wiki moja baadae wakati hawana kitu wanafanya Dar es Salaam.

Tangu Yanga Princess wagome kuvunja kambi hakuna kiongozi yeyote aliyewatembelea kuwapa muongozo wa klabu hivyo wengi wao wanazagaa mitaa ya Mikocheni ilipo kambi yao.

SOMA NA HII  YANGA YATUMIA MUDA KUWASOMA WAPINZANI WAO, KAZI INAENDELEA