Home Simba SC SIMBA SC WAISHINDA AL MERRIKH CAF

SIMBA SC WAISHINDA AL MERRIKH CAF


Bodi ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeisafisha Simba juu ya tuhuma zilizoibuliwa na Al Merrikh ya Sudan ya kuwapa majibu ya uongo ya Covid-19 wachezaji wake nane wa kikosi cha kwanza kabla ya mechi baina yao iliyochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 16.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Nidhamu ya CAF, Raymond Hack imeeleza kuwa vielelezo vilivyowasilishwa na Al Merrikh kuituhumu Simba ni batili na vimekosa uhalali wa kuitia hatiani.

“Tungependa kuthibitisha kuwa malalamiko ya Al Merrikh kuhusu mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika namba 101, yamepokelewa. Hata hivyo kanuni na muongozo wa sasa ufafanua hivi, vipimo vya PCR vinatakiwa kwa watakaoshiriki mechi ndani ya muda usiozidi saa 48 kabla ya mchezo.

Majibu yatakayotolewa kabla ya mechi ndio rasmi na ndiyo yatatoa uhalali wa wachezaji kama unavyofahamu majibu yanaweza kutofauti kutoka siku moja hadi nyingine.

Lakini pia wachezaji kadhaa wa Simba walipimwa na kuonekana wameambukizwa kama ilivyo kwa maofisa wa CAF,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ya CAF imeeleza pia kuwa uchunguzi uliofanywa na Bodi yake ya nidhamu umebaini kuwa kwa mujibu wa utaratibu wa vipimo wa Tanzania, majibu ya vipimo hayatolewi kwa watu waliobainika kuambukizwa Covid-19 na badala yake huwa kwa wale ambao hawajaambukizwa

“Kwa hiyo tungependa kuthibitisha kwamba majibu ya Covid-19 yaliyowasilishwa na CAF ndiyo yatapewa kipaumbele kwenye suala linalohusu mechi ya Simba dhidi ya Al Merrikh,” imesema taarifa hiyo.

Wiki mbili zilizopita, Al Merrikh ilidai kuwa wachezaji wake nane walipewa majibu ya uongo ya Covid-19 ambayo yalionesha wameambukizwa wakidai hawakuwa wameambukizwa.

Wachezaji hao ni Abdelrahman Isaac, Bakhit Khamis, Ahmed Abdelmoneim, Tajeddin Yaqoub, Ramadan Ajab, Tony Edjomariegwe, Bakri Al Madina, and Saif Ad Damazin

SOMA NA HII  KIPA ALIYECHEZA NA MASTAA WAKUBWA DUNIA AFUNGUKA DILI LAKE LA KUJA SIMBA....