Home Simba SC SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA AL MERRIKH, MCHEZO UTAKUWA MGUMU

SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA AL MERRIKH, MCHEZO UTAKUWA MGUMU

 NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa mchezo wao wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Merrikh ya Sudan utakuwa mgumu ila wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya.

Kesho Machi 16, Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Al Merrikh ambayo nayo imeweka wazi kwamba inahitaji hizo pointi tatu Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Al Hilal, Sudan ubao ulisoma Al Merrikh 0-0 Simbaa na kuwafanya wagawane pointi mojamoja na kesho watakutana tena ukiwa ni mchezo wa pili.

Bocco amesema”Tupo nyumbani na tupo tayari kupambana kwa ajili ya timu na kupata alama tatu. Tunashukuru kwa ushirikiano tunaopata kwa mashabiki ingawa tunajua kwamba kesho hawatakuwepo uwanjani.

“licha ya kwamba hawatakuwepo uwanjani lakini tunaamini kwa dua zao tutapata ushindi, ushindani ni mkubwa wapinzani wetu tunawaheshimu kwa kuwa ni timu nzuri na inaleta ushindani,” .
Kundi A Simba inaongoza ikiwa na pointi 7 na Al Merrikh ina pointi moja ikiwa nafasi ya nne.

Mchezo wa kesho utaanza kutoa picha namna kundi A litakavyokuwa kwa kuwa mpaka sasa kundi lipo wazi na hakuna mwenye uhakika wa kutinga robo fainali mpaka pale ambapo atashinda mechi zake.
SOMA NA HII  BAADA YA 'KUMVUTISHA PUNZI YA JOTO' MSAUZI JANA....UONGOZI SIMBA WATOA NENO HILI KWA MASHABIKI...