Home news TANZIA:RAIS MAGUFULI ATANGULIA MBELE ZA HAKI

TANZIA:RAIS MAGUFULI ATANGULIA MBELE ZA HAKI


 TANZIA

RAIS wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  John Pombe Magufuli amefariki dunia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Samia Suluhu ametangaza msiba wa Rais, John Pombe Magufuli.


Samia usiku wa kuamkia leo kupitia television ya Taifa ya Tanzania,  TBC amesema kuwa umauti umemkuta Magufuli alipokuwa akipatiwa matibabu.


Ameongeza kwa kusema kuwa Magufuli ametangulia mbele za haki kutokana na tatizo la moyo alilokuwa nalo  muda mrefu.


Utaratibu wa kumpumzisha Magufuli utatolewa na Serikali ambapo kutakuwa na maombolezo ya siku 14 na bendera zitakuwa nusu mlingoti.

Magufuli atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwa Tanzania na jitihada zake katika kila sekta ikiwa ni pamoja na michezo. 


Pumzika kwa Amani

SOMA NA HII  WAKATI MASHABIKI WA GEITA GOLD WAKISEMA WATAISUSA TIMU....'FEI TOTO' NA FARID WAWAANGUKIA YANGA....