Home Yanga SC KOCHA YANGA AANZA NA KUTATUA TATIZO LA UBUTU WA SARPONG

KOCHA YANGA AANZA NA KUTATUA TATIZO LA UBUTU WA SARPONG


 KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi ameamua kulifanyia kazi tatizo linalomfanya kutokufunga straika wa timu hiyo, Michael Sarpong kwa kumpa mazoezi ya kufumania nyavu kila mara ili aweze kuondoa wasiwasi ambao unatajwa kuwa ndiyo uchawi pekee na chanzo cha kushuka kwa ufungaji wake.

 

Sarpong alisajiliwa na Yanga, akitokea Rayon Sports ya Rwanda, ambapo hadi sasa amefanikiwa kufunga mabao 4 kwenye Ligi Kuu Bara, jambo linalowafanya mabosi wake wa Yanga na mashabiki kutofurahishwa na mwenendo wa ufungaji wake ambapo sasa kocha wake, Mwambusi ameamua kumtibu.

 

Habari zimeeleza kuwa, tayari Mwambusi ameamua kulivalia njumu suala la ubutu wa mabao katika kikosi hicho, kwa kumpa muda mwingi wa kufanya mazoezi ya kufunga sambamba na wachezaji wenzake kama Fiston Abdoul Razack na Yacouba Sogne.


β€œKuna uwezekano mkubwa wa ligi kurejea Sarpong akaanza kutupia kila mechi, maana kocha Mwambusi ameshagundua tatizo lake hilo ambapo tayari kwenye mazoezi yake ameonekana akiwahimiza zaidi mastraika wote kuhakikisha wanafanyia mazoezi ya kina katika suala hilo la ufungaji ili kuondoa ukame wa mabao tena,” kilisema chanzo hicho.

 

Akizungumzia hilo Mwambusi ambaye amechukua mikoba ya Cedric Kaze alisema: β€œProgram zangu zote moja ya lengo ni kuhakikisha nafanyia kazi safu ya ushambuliaji na kwa sasa naangalia utimamu wa mwili kwa mchezaji mmoja mmoja na baada ya hapo nitatengeneza muunganiko wa jumla ili ligi itaporudi tatizo liwe limekwisha.”


Chanzo: Championi

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUPOTEANA ZNZ...SENZO AIBUKA HADHARANI NA KUIMWAGIA 'HEKO' SIMBA..