Home Yanga SC YANGA NA DAKIKA 180 ZA MOTO BONGO

YANGA NA DAKIKA 180 ZA MOTO BONGO


  
CEDRIC Kaze baada ya kubwana mbavu mbele ya Mbeya City kwa kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili ana dakika 180 za moto kufunga mwezi Februari.


Februari 13, Yanga ilikubali sare hiyo ambapo bao la Yanga lilifungwa na Deus Kaseke huku lile la Mbeya City likifungwa na Athanas Pastory kwa mkwaju wa penalti.

Leo Yanga itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku.

Kaze amesema kuwa atapambana kuwarejesha wachezaji wake kwenye morali waliokuwa nao ili kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja.

“Ligi ni ngumu na kila timu inahitaji pointi tatu hivyo tutajitahidi kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo kwa kuwa wachezaji wapo tayari kupata matokeo chanya,”.

iIkimaliza hesabu za dakika 90 leo mbele ya Kagera Sugar ambayo kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ilishinda bao 1-0 la Mukoko Tonombe kwa pasi ya Tuisila Kisinda ina kibarua kingine tena kwa Mkapa.

Itakuwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar itakamilisha dakika 180 za Kaze kupiga hesabu zake za mwezi,ambapo itakuwa ni Februari 20, Uwanja wa Mkapa. Inakumbuka kwamba ilipokutana nao Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ilishinda kwa bao 1-0.

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 19 imekusanya jumla ya pointi 45 huku wapinzani wao Simba wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 39 baada ya kucheza mechi 17.

SOMA NA HII  MAPYA YAIBUKA JANGWANI...HARMONIZE "SITOISHABIKIA TENA YANGA SC