Home Habari za michezo KIEMBA:- “SIMBA WAMECHEZA MECHI NYEPESI SANA…”,HUWEZI KUMFUNGA AL AHLY KIRAHISI HIVYO…

KIEMBA:- “SIMBA WAMECHEZA MECHI NYEPESI SANA…”,HUWEZI KUMFUNGA AL AHLY KIRAHISI HIVYO…

Habari za Simba

Mchambuzi wa soka nchini Amri Kiemba amesema mechi mbili za kirafiki alizocheza Simba SC ni nyepesi kulinganisha na mashindano yaliyopo mbele yao.

Mchambuzi huyo ameenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, licha ya kuwa ni nyepesi lakini ina maana kwa mwalimu Roberto Oliviera ‘Robertinho’.

“Ni mechi nyepesi kulinganisha na michuano ambayo wanacheza lakini kiualimu inasaidia kutengeneza kile ambacho unataka kutokana na ushindani mdogo ina maana kama washambuliaji wako wamepoteza uwezo wa kufunga wanaweza kufunga na kuanza kugain kujiamini.

“Inawezekana mwalimu ana wazo lakini wachezaji hawamini katika ilo wazo lakini kama mnacheza na timu za kati inafanya wachezaji wazoee hizo mbinu, kama mnacheza mechi ngumu na mnafungwa inaleta ugumu kwa wachezaji kuamini hizo mbinu na kufanya mpango kufeli,” alisema Kiemba.

Simba wamecheza dhidi ya Cosmopolitan FC na kushinda 5- 1 lakini awali pia walicheza na Kipanga FC wakashinda 3-0.

SOMA NA HII  TUSIPOTEZE MUDA...HAWA QATAR NI KAMA TAIFA STARS TU...TOFAUTI YAO NA SISI NI UTAJIRI TU..