Home news UNAMKUMBUKA SARPONG…?UNAAMBIWA KASAJILIWA TENA HUKO KWA KELELE KAMA ZOTE….

UNAMKUMBUKA SARPONG…?UNAAMBIWA KASAJILIWA TENA HUKO KWA KELELE KAMA ZOTE….


MSHAMBULIAJI wa Zamani wa Yanga, Mghana Michael Sarpong amejiunga rasmi na timu ya AS Kigali inayoshiriki Ligi Kuu Rwanda (RNFL), akitokea Al Nahda Saudi FC ya Uarabuni.

Sarpong aliyeichezea Yanga msimu wa 2020-2021, kutua kwake AS Kigali kunamfanya kukutana na wachezaji wawili waliocheza wote Yanga, Mnyarwanda Haruna Niyonzima na Mghana Lamine Moro wanaokipiga ndani ya Klabu hiyo.

Hata hivyo sio kwa mara ya kwanza kwa Sarpong kucheza RNFL kwani kabla ya kujiunga na Yanga alikuwa akiichezea Rayon Sports, moja ya timu yenye mashabiki wengi nchini Rwanda.

Baada ya kujiunga na timu hiyo, Sarpong  amesema ataipambania timu na kuhakikisha inafikia malengo iliyojiwekea.

β€œNimekuja hapa kufanya kazi, nitajituma sana kwa kushirikiana na wenzangu ili tufikie malengo ya timu,” alisema Sarpong aliyekabidhiwa jezi namba 23.

Katika RNFL, AS Kigali ipo nafasi ya tano, baada ya kucheza mechi 19 na kuvuna pointi 31 ikiwa imeshinda nane, sare saba na kupoteza nne.

SOMA NA HII  POLISI TANZANIA WAANZA KUIVUTIA KASI SIMBA