Home news WAAMUZI HAWA WAWEKA REKODI MBELE YA RAIS MAGUFULI

WAAMUZI HAWA WAWEKA REKODI MBELE YA RAIS MAGUFULI

 


FROLENTINA Zabron, mwamuzi wa soka ndani ya ardhi ya Tanzania anashikilia rekodi ya kuwa mwamuzi wa kwanza kuongoza mchezo wa Ligi Kuu Bara mbele ya Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ambaye ametangulia mbele za haki Machi 17 alikuwa ni mpenda michezo na aliweka wazi kuwa alikwenda hapo kwa ajili ya heshima ya watu wa michezo pamoja na taifa la Tanzania.

Dakika 90 zilikamilika Mei 19 kwa Simba kufungwa bao 1-0 na Kagera Sugar na Magufuli alisema kuwa kwa mpira ambao aliona wakicheza Simba itakuwa ngumu kwao kuleta taji la Afrika katika ardhi ya Tanzania.

Pia, Martin Saanya alikuwa mwamuzi wa mchezo wa Yanga dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa ulikuwa ni wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huu ulikuwa ni dabi ya kwanza kwa Rais John Magufuli kufika uwanjani na alishuhudia Simba ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0. Ilikuwa ni Machi 8, 2020.

Wengine ambao walikuwa wasaidizi wake ilikuwa ni pamoja na Hery Sasii, Abdalah Mwinyimkuu, Frank Komba.

 

SOMA NA HII  KUELEKEA SIKU YA WANANCHI...YANGA HAWATAKI DENI AISEEE...WAALIZANA KIMYA KIMYA NA MAYELE...DILI LA SAUZI LAFAA..