Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WASUDAN LEO…MORRISON SURE BOY WAWEKWA NNJE YANGA…KAZE AFUNGUKA A-Z...

KUELEKEA MECHI NA WASUDAN LEO…MORRISON SURE BOY WAWEKWA NNJE YANGA…KAZE AFUNGUKA A-Z ISHU ILIVYOKUWA…


Klabu ya mwisho ya Yanga yamemalizika jana jioni kuelekea kuikabili Zalan FC siku ya leo kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, wachezaji na benchi la ufundi lakiri kumaliza mazoezi salama na wako tayari kuipambania nembo ya timu hiyo.

Mechi ya Zalan FC dhidi ya Yanga SC itapigwa mijira ya saa 10:00 Jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumzia maandalizi hayo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amesema maandalizi yalikuwa mafupi kutokana na kwamba walibanwa na ratiba ya mechi ya Ligi waliocheza Jumanne iliyopita dhidi ya Azam FC huku akiongeza kuwa maandalizi kwa sasa yako vizuri kuanzia mazoezi mpaka kisaikolojia kwa ajili ya kuwakabili Wasudan Kusini.

“Maandalizi ya kikosi ni mazuri japo hatuwajui sana wapinzani wetu Zalan ni timu ya aina gani na wanachezaje, lakini tutatumia dakika za mwanzo kuwasoma na kuona tunawakabili kwa mbinu gani kupata matokeo.

“Bernard Morrison aliumia kwenye mechi ya Azam, Sure Boy naye alikuwa na majeraha lakini yameongezeka zaidi zaidi kwa hiyo uwezekano wa kuwatumia hawa wachezaji ni mdogo sana na huenda wakakosekana kwenye mchezo huo.

“Dickson Job naye aliumia lakini ameanza mazoezi jana (juzi) na leo (jana), kwa hiyo anaendelea vizuri huenda akawa kikosini. Lazarous Kambole amerejea na tunaona anafanya vizuri mazoezini, huenda naye alatusaidia lakini maamuzi yatatoka leo kutoka kwenye benchi la ufundi.

“Mwaka jana hatukufanya vizuri kimataifa kwa hiyo tumejipanga mwaka huu kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi. Tunawaomba mashabiki waje kutusapoti,” amesema Kaze.

SOMA NA HII  KISA USAJILI WA MASTAA WAPYA NA MZUNGU JUU....RAGE AIBUKA NA JIPYA KUHUSU HATMA YA SIMBA MSIMU UJAO...