Home Uncategorized EMMANUEL OKWI AMETIMIZA MIAKA 28

EMMANUEL OKWI AMETIMIZA MIAKA 28

 


NYOTA wa Klabu ya Al Ittihad na timu ya Taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi ambaye ni mshambuliaji leo anatimiza miaka 28.

Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia,  Okwi ameletwa duniani Desemba 25,1992 huko nchini Uganda.

Kwenye maisha yake ya soka aliweza kupita ndani ya Klabu za Simba na Yanga kwa nyakati tofautitofauti.

Alisajiliwa na Simba msimu wa 2010-13 akitokea Klabu ya SC Villa ambapo alikuwa amecheza jumla ya mechi 40 na kutupia mabao 13.

Msimu wake wa kwanza ndani ya Simba alicheza jumla ya mechi 38 na kutupia mabao 18, alisepa Simba na kujiunga na Klabu ya Etoile du Sahel msimu wa 2013 hakudumu akajiunga na SC Villa kisha Yanga msimu wa 2013-14 ambapo alicheza jumla ya mechi 18 na kutupia mabao 9.


Alirejea tena ndani ya Simba msimu wa 2017-19 ambapo alicheza jumla ya mechi 53 na kutupia mabao 36 kwa sasa yupo ndani ya Al Ittihad ya Misri ambapo amecheza jumla ya mechi 14 na kutupia mabao mawili.


SOMA NA HII  KAMA UTANI VILE KOCHA NAMUNGO ABWAGA MANYANGA