Home Yanga SC YANGA PRINCESS YAUPIGIA HESABU UBINGWA WA SIMBA QUEENS

YANGA PRINCESS YAUPIGIA HESABU UBINGWA WA SIMBA QUEENS


 KOCHA Mkuu wa Klabu ya Yanga Princess, Edna Lema amefunguka kuwa, mpaka sasa bado hakuna uhakika wa bingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake, licha ya tofauti ya pointi moja Simba Queens.

 

Yanga Princess walipoteza uongozi wa ligi baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam.

 

Simba inaongoza msimamo ikiwa na pointi 39, huku Yanga Princess wao wakiwa katika nafasi ya pili na pointi zao 38 baada ya wote kucheza mechi 15 


 Edna amesema:“Bado kikosi changu kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri msimu huu na ikiwezekana kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake licha ya kwamba tuko nyuma kwa pointi na viongozi wa msimamo Simba Queens.

 

“Pointi moja kwenye soka ni ndogo sana na lolote linaweza kutokea hivyo kila mtu acheze na kushinda mechi zake, kuhusu bingwa tutamjua mwishoni.


“Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na kutimiza lengo letu la kutwaa ubingwa hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti matumaini yapo na inawezekana,” .


Bingwa mtetezi wa taji hilo kwa sasa ni kinara Simba Queens ambaye alitwaa taji hilo msimu uliopita.


SOMA NA HII  YANGA KUWAVUTA NYOTA WAWILI KUTOKA TUNISIA