Home Habari za michezo KISA KIPIGO CHA JANA DHIDI YA UGANDA….KOCHA TAIFA STARS ATOKOMEA GHAFLA…

KISA KIPIGO CHA JANA DHIDI YA UGANDA….KOCHA TAIFA STARS ATOKOMEA GHAFLA…

Taifa Stars

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Adel Amrouche ametokomea kusikojulikana baada ya mchezo wa timu yake na Uganda kumalizika jana Jumanne, Machi 28, 2023 wakati kikosi chake kikiambulia kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa kufuzu Fainali za AFCON 2023.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Adel aliwakimbia wanahabari huku kocha Mkuu wa Uganda, Milutin Sredojević akibakia peke yake kwenye chumba na wanahabari.

Inadaiwa kuwa huenda kocha huyo alichukizwa na matokeo hayo ya dakika za nyongeza ambayo yalitokana na bao Rogers Mato Kassim dakika ya 90+1’ akitokea benchi katika Dimba la Mkapa, wakati mchezo wa awali, Stars iliifunga Uganda nchini Misri.

Katika Kundi F la michuano hiyo, Algeria ndiyo inaongoza ikiwa na alama 12, Tanzania na Uganda wana alama 4 kila mmoja na Niger ina alama 2 wakati mechi mbili zikiwa zimesalia kwa kila timu.

Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kuhusu kilichotokea mpaka Amrouche akashindwa kujumuika na Micho kwenye mahojiano na wanahabari baada ya mechi kumalizika.

SOMA NA HII  AHMED ALLY:- MAMBO MAKUBWA HUFANYIKA USIKU...HAKUNA WAKUTUZUIA...