Home Habari za michezo BAADA YA KUVAA UZI WA TIMU YA TAIFA YA CONGO…MAYELE AFUNGUKA MAPYA…ATAJA...

BAADA YA KUVAA UZI WA TIMU YA TAIFA YA CONGO…MAYELE AFUNGUKA MAPYA…ATAJA UGUMU WAKE…

Habari za Yanga

Mara baada ya kufanikiwa kupata nafasi ya kucheza dakika tatu za mwisho katika kikosi cha Timu ya Taifa ya DR Congo, Fiston Mayele ameelezea furaha yake, huku akisema tukio hilo limempa nguvu mpya ya kupambana.

DR Congo katika mchezo wa juzi Ijumaa wa kufuzu AFCON, ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mauritania, mechi ikichezwa Uwanja wa TP Mazembe, Lumbumbashi, DR Congo. Mayele aliingia dakika ya 87 akichukua nafasi ya Cedric Bakambu.

Akizungumza nasi, Mayele alisema: “Ni tukio kubwa sana katika maisha yangu ya mpira kuichezea timu ya taifa ya DR Congo, hii ilikuwa ni ndoto kubwa sana kwangu na nashukuru imetimia, hii imeniongezea pia nguvu ya kuendelea kupambana ili nipate kuitwa mara kwa mara.

“Najua sio kazi rahisi kuitwa mara kwa mara katika timu ya taifa kutokana na ubora wa wachezaji waliopo katika nafasi yangu, lakini lazima nitahakikisha napambana ndani ya timu yangu, naamini nitafanikiwa.”

SOMA NA HII  SIMBA WAKUBALI KUPITIA MAGUMU...WANAJIPANGA UPYA