Home Yanga SC YANGA PRINCESS: TUPO KAMILI

YANGA PRINCESS: TUPO KAMILI

 


KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga Princess, Edina Lema amesema kuwa ana imani na maendeleo ya nyota wake, na matumaini makubwa watarudi kwa nguvu na kuhakikisha wanafanya vizuri.

Edina Lema amefanikiwa kuiongoza Yanga Princess kwenye michezo 15 ambapo wamekusanya pointi 38 zinazowaweka katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi.

Akizungumzia mipango yao, Lema alisema: “Kikosi chetu kwa sasa kimesitisha mazoezi mpaka pale shughuli zote za mazishi ya Hayati Rais Dk John Magufuli.

“Lakini nimepata nafasi ya kuwaona nyota wangu ambao wanaonekana kuwa tayari hivyo nina imani tutajipanga na kufanya vizuri,”


 

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUONGOZA LIGI...NABI KAKITAZAMA KIKOSI CHAKE WEE..KISHA AKATOA OMBI HILI YANGA...