Namungo FC

NAMUNGO FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA NKANA

admin April 3, 2021 8:47 am

 


HEMED Morocco, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Nkana FC ya Zambia na wanahitaji pointi tatu.

Namungo ipo kundi D, imecheza mechi mbili na kupoteza zote, ilianza kupoteza mbele ya Raja Casablanca bao 1-0 ugenini na ikapoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Pyramids, Uwanja wa Mkapa.

Inakutana na Nkana FC ambayo nayo haijakusanya pointi baada ya kupoteza mechi zake zote mbili kwenye makundi jambo ambalo litaongeza ugumu kwenye mchezo huo.

Morocco amesema  alikusanya makosa kwenye mechi zilizopita jambo ambalo litawafanya waingie uwanjani kwa namna nyingine.

 “Makosa kwenye mechi zetu ambazo zimepita yanatufanya tuingie kwa hesabu za tofauti kukutana na wapinzani wetu ambao tunawaheshimu ila kwa kuwa tupo nyumbani hatuna mashaka.

“Wachezaji wana morali kubwa na nimewaambia kwamba wanapaswa wajiamini kila kitu kinawezekana. Ushindi ambao tutapata ni muhimu kwa timu na Tanzania kiujumla,” amesema.

KIKOSI CHA SIMBA KINACHOTARAJIWA  LEO DHIDI YA AS VITA MANULA : – TUNATATAKA KUWEKA REKODI NGUMU KUFUTIKA CAF

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply