Ligi Kuu

KOCHA MTIBWA SUGAR ATAJA SABABU YA KUGOMA KURUDI BONGO

admin April 10, 2021 10:47 am

 


HITIMANA Thiery,  Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kikubwa kinachomfanya asifikirie kurejea Bongo ni kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya viongozi. 


Thiery amesema kuwa kwa sasa yupo Rwanda akiendelea kufanya mambo yake ikiwa mambo yatakwenda sawa anaweza kufikiria kurudi Tanzania. 

Kwa sasa Mtibwa Sugar ipo mikononi mwa Kaimu Kocha Msaidizi, Vincent Barnaba ambaye jana aliongoza kikosi hicho mbele ya Azam FC. 


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex,  ubao ulisoma Azam FC 2-0 Mtibwa Sugar na mabao yote yalifungwa na Prince Dube. 


Thiery amesema:”Nipo Rwanda na sifikirii kurudi Tanzania kwani hatukuwa na maelewano mazuri na baadhi ya viongozi hayakuwa vizuri na hata viongozi wenyewe walikuwa wanajua,”.

SIMBA: KAZI INAENDELEA, TUKUTANE ROBO FAINALI PILATO WA AL AHLY V SIMBA ATOA KADI NNE, TATU ZA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply