Azam FC

AZAM FC BADO HAWAJAKATA TAMAA KUHUSU UBINGWA WA LIGI KUU BARA

admin April 18, 2021 3:47 pm


 VIVIER Bahati, kocha msaidizi wa Azam FC amesema kuwa bado hawajakata tamaa kwenye mbio za kusaka ubingwa kwa kuwa nafasi bado ipo.

Azam FC ipo ndani ya tatu bora na ilianza kwa kasi msimu huu wa 2020/21 jambo lililowafanya waje na sera yao kwamba wana jambo lao.

Kwa sasa ipo mkoani Dodoma ikiwa inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji, unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu ina pointi 50 baada ya kucheza mechi 26, nafasi ya pili ni Simba wenye pointi 52 baada ya kucheza mechi 22 na Yanga ni namba moja na pointi zao 54 baada ya kucheza mechi 25.

Bahati amesema:”Bado tuna mechi mkononi na kila mmoja kwa sasa anajua kwamba ushindani ni mkubwa nasi tunahitaji kupata matokeo mazuri.

“Malengo yetu ni kuona kwamba tunapambana ili kupata ushindi na kufikia malengo ya kutwaa ubingwa,” .

MWADUI YAPOTEZA MBELE YA SIMBA, BOCCO AWALIZA KWA KICHWA USIPANGE KUKOSA NAKALA YAKO YA CHAMPIONI JUMATATU, JOB ANA NENO LAKE ,MJUE STAA ALIYEKIMBIA FAMILIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply