Simba SC

BREAKING: LUIS MIQUISSONE ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA

admin April 19, 2021 1:47 pm


 MCHEZAJI wa Simba, Luis Miquissone ameteuliwa kuwa mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara kwa mwezi Machi.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Bara, TPLB imemtambulisha nyota huyo kuwa mchezaji bora ndani ya Machi.

Kiungo huyo amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Anakumbukwa kwa kupachika bao la dakika za lala salama mbele ya Tanzania Prisons ambalo liliwapa pointi moja mabingwa hao watetezi kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

Amewashinda Idd Seleman, ‘Nado’ wa Azam FC na Paul Nonga wa Gwambina FC.

Luis kwa mwezi Machi aliweza kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao.

MAMELOD SUNDOWNS WAJIPANGA KUMSAJILI MANULA KAMA MRITHI WA ONYANGO YANGA: MCHEZO WETU WA KESHO DHIDI YA GWAMBINA UTAKUWA MGUMU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply