Home kimataifa UEFA YAPINGA KUANZISHWA KWA EUROPEAN SUPER LEAGUE

UEFA YAPINGA KUANZISHWA KWA EUROPEAN SUPER LEAGUE

 


SHIRIKISHO la Soka Barani Ulaya limepinga kuanzishwa kwa Ligi mpya Barani humo itakayoitwa ‘European Super League’ mashindano ambayo yatakuwa yakifanyika katikati ya wiki.

 

 

Ni vilabu 12 vya mpira wa miguu zinazoongoza Ulaya zimekutana na kutangaza wamekubali kuanzisha mashindano hayo mapya.

 

 

Vilabu vilivyokubali mpaka sasa ni AC Milan, Arsenal FC, Atlético de Madrid, Chelsea FC, FC Barcelona, FC Internazionale Milano, Juventus FC, Liverpool FC, Manchester City, Manchester United, Real Madrid CF na Tottenham huku vilabu vitatu vikitarajiwa kuongezeka lakini PSG, Bayern na Borrusia Dortmund wamekataa kujiunga katika Ligi hiyo.

 

TAARIFA YA UEFA KUPINGA ‘EUROPEAN SUPER LEAGUE’


“Tutachukua hatua zote zinazowezekana kwetu, katika viwango vyote, kimahakama na michezo ili kuzuia kutokea. Kandanda inategemea mashindano ya wazi na sifa ya mchezo; haiwezi kuwa kwa njia nyingine yoyote.

 

“Klabu zinazohusika zitapigwa marufuku kucheza kwenye mashindano mengine yoyote katika ngazi ya ndani, Ulaya au ulimwengu, na wachezaji wao wanaweza kunyimwa nafasi ya kuwakilisha timu zao za kitaifa.”

SOMA NA HII  FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA YAWEZA KUPIGWA WEMBLEY