Beki mkongwe wa Simba SC na raia wa Kenya Joash Onyango anatakiwa na timu kubwa za Afrika Kusini.
Taarifa kutoka Afrika Kusini zinasema kuwa , uwezo mkubwa wa beki huyo pamoja na kucheza kwa juhudi uwanjani umezifanya klabu za Oralando Pirates na Kazier Chiefs kuangalia uwezekano wa kumsajili.
Chanzo kutoka huko,kinasema kuwa klabu ya Oralando Pirates wameonyesha nia zaidi ya kumsajili neki huyo, huku wakipanga kutoa ofa ya Dola Milioni moja sawa na bilioni 2 za kitanzania kwa klabu yake ya sasa Simba SC.
Onyango ambaye amejiunga na Simba SC, msimu huu akitokea Gor Mahia ya Kenya, amekuwa sehemu ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Simba SC.
Katika msimu huu wake wa kwanza ndani ya Simba SC, Onyango amefanikiwa kuiwezesha Simba SC kufika hatua ya robo fainali ya mashindano ya Klabi Bingwa Afrika.
Aidha, uimara wa safi ya ulinzi ya Simba SC kwa msimuu huu imeonekana kuimarika zaidi ya misimu kadhaa ya nyuma.
Katika kikosi cha Simba SC, Onyango amefanikiwa kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza ambapo amekuwa akicheza sambamba na Sergio Wawa.
Hii si mara ya kwanza wachezaji wa Simba SC kuzivutia timu za Afrika Kusini, kwani mapema hivi karibuni Klabu bingwa nchini huko, Mamelod Sundowns iliweka wazi nia ya kumsajili golikipa namba moja wa Simba SC , Aishi Manula.