Simba SC

ISHU YA MOHAMED HUSSEIN KWENDA YANGA, SIMBA WAFUNGUKIA

admin April 23, 2021 3:47 am

 MTENDAJI Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa nyota wao  Mohamed Hussein bado yupo ndani ya Simba kwa sasa na hatokwenda Yanga.

Imekuwa ikielezwa kuwa nahodha huyo msaidizi yupo kwenye mazungumzo na Yanga ambayo inahitaji kuboresha kikosi chake.

Mkataba wa Hussein ambaye ni beki mzawa inaelezwa kuwa mkataba wake umebaki muda wa mwezi mmoja kuisha.

“Tumeskia hizo taarifa za beki ba nahodha wetu kutaka kusajiliwa Yanga, lakini nipende kuwaweka wazi kuwa huyo bado ni mchezaji wetu kwa kuwa ana mkataba na Simba.

“Lakini pia uongozi una matarajio makubwa ya kumpa mkataba mpya wa kuendelea kusalia ndani ya Klabu yetu,”.

Chanzo: Championi

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA CV YA KOCHA MPYA WA VIUNGO YANGA HII HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply