Simba SC

SIMBA KITUO KINACHOFUATA NI GWAMBINA

admin April 23, 2021 5:47 am

 


BAADA ya kumaliza kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar kikosi cha Simba kimetua Mwanza kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC.

Ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-2 Simba ambapo watupiaji walikuwa ni Luis Miquissone na Chris Mugalu. 

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa kesho, Aprili 24, Uwanja wa Gwambina Complex.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 3-0 Gwambina FC na kufanya wapinzani hao kuacha pointi tatu kwa Mkapa.

Kwenye msimamo wa ligi, Simba ipo nafasi ya pili na ina pointi 55 baada ya kucheza mechi 23 huku Gwambina FC ikiwa nafasi ya 12 na ina pointi 30 baada ya kucheza mechi 25.

KIGOGO WA SUPER LEAGUE AKOMAA EXCLUSIVE: KOCHA WA VIUNGO WA YANGA ATAJA NAMNA ATAKAVYOFANYA KAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply