Home Simba SC CHAMA AWEKA REKODI YA PASI ZA MWISHO BONGO

CHAMA AWEKA REKODI YA PASI ZA MWISHO BONGO

 NYOTA wa Simba Clatous Chama ameweka rekodi ya kuwa namba moja kwa wanaotengeneza pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar,  Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikifikisha jumla ya pointi 49 Chama amefikisha pasi 10.

Mbali na kuwa na pasi 10 pia nyota huyo ametupia jumla ya mabao 7 kwa msimu huu akiwa ni moja ya viungo bora wanaofanya vizuri ndani ya ligi.

Anayemfuata kwa kuwa na pasi nyingi za mwisho ni Luis Miquissone ambaye naye anacheza  Simba akiwa na pasi 9 za mabao.

David Luhende wa Kagera Sugar beki mzawa ambaye ana pasi nyingi za mabao akiwa nazo 7 pia ana bao moja.

SOMA NA HII  TRY AGAIN : MSIMU UJAO SIMBA SC TUTAKUWA NA KIKOSI BORA ZAIDI