Home Simba SC HD : ILIBAKI KIDOGO TU NINGERUDI YANGA

HD : ILIBAKI KIDOGO TU NINGERUDI YANGA

[the_ad id="25893"]


Kama sio kubadili mawazo dakika za jioni ni dhahiri kwa sasa kiungo nyota wa Simba, Hassan Dilunga ‘HD’ angekuwa akitinga uzi wenye rangi wa kijana na njano, baada ya kufichua ilibaki kidogo tu atue Jangwani.

Kiungo mshambuliaji huyo amefichua, kabla ya kuongeza mkataba mpya Msimbazi alikuwa amefanya mazungumzo na viongozi wa Yanga ili asaini mkataba, lakini akaamua kuwapiga chini ili kuendelea kuitumia timu hiyo iliyomsajili kutoka Mtibwa Sugar misimu mitatu iliyopita.

Dilunga alisema mara baada ya mkataba wake wa miaka miwili na Simba kumalizika, alifuatwa na Yanga walionyesha nia ya kutaka kumsajili, wakati huo akisikilizia mabosi wa Msimbazi kama watamwongezea mkataba mpya au la!

Alisema alikaa chini na viongozi hao wa Jangwani katika eneo moja tulivu wakizungumza ili wamsajili na kumpatia mkataba wa miaka miwili kwenda kuwatumikia timu yao ya Yanga.

“Tulikubaliana muda wa mkataba uwe wa miaka miwili pamoja na pesa niliyotaka wanipatie waliniambia wapo tayari kunipa, lakini nilishangaa siku zinakwenda bila ya kutimiza kile tulichofikia mwisho na kukubaliana,” alisema Dilunga aliyeifungia Simba jumla ya mabao 11 tangu ajiunge nayo, yakiwamo mawili ya msimu huu na saba msimu uliopita.

“Baada ya kuona siku zinazidi kusonga mbele na hakuna lolote linalofanyika dhidi ya viongozi wa Yanga katika yale tuliyokubaliana niliona wanazingua na hawapo siriasi katika suala hilo na baada ya mabosi wangu kuniambia wapo tayari kuniongezea mkataba mpya sikuwa na hiyana.

“Nawaheshimu waajiri wangu Simba hawakutaka maneno mengi kama ilivyokuwa kwa Yanga kile tulicgokubaliana na nilikuwa nahitaji katika mkataba wangu huu mpya baada ya muda mchache walilipatia na kusaini tena kwa miaka miwili nikitumikia hadi sasa.”

Alisema kilichowakwamisha Yanga kumpa ni dau la fedha walilokubaliana, hiyo ni mara ya pili kumkosa kwani kabla ya kutua Msimbazi walitaka kumrejesha Jangwani, lakini wakazembea na kwenye Simba. Kumbuka Dilunga alishaichezea Yanga hapo awali kabla ya kwenda Stand United na kisha kurudi Mtibwa Sugar aliyoichezea mara ya mwisho 2017-2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here