Home Simba SC MFARANSA WA SIMBA ACHEKELEA KUANZA NA MABAO MATATU CAF

MFARANSA WA SIMBA ACHEKELEA KUANZA NA MABAO MATATU CAF


  
DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amechekelea kuanza kazi na nyota wake wawili ambao wamehusika kwenye mabao matatu katika Ligi ya Mabingwa Afrika yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) hatua ya makundi.

Simba ikiwa imecheza mechi nne na kuongoza kundi A na pointi zake 10, imefunga jumla ya mabao matano, mawili yamefungwa na Luis Miquissone raia wa Msumbiji, Chris Mugalu raia wa Congo na Mohamed Hussein, ‘Zimbwe’ ambaye ni Mzawa.

Katika wafungaji hao wa mabao, Gomes ameanza kufanya mazoezi na Mugalu ambaye amefunga mabao mawili na mtengeneza mipango Bernard Morrison ambaye ana pasi moja ya bao alitoa kwenye mchezo dhidi ya Al Merrikh bao lilifungwa na mshikaji wake Zimbwe.

Mugalu alifunga bao la kwanza mbele ya AS Vita ugenini kwa mkwaju wa penalti na bao lake la pili alifunga Uwanja wa Mkapa mbele ya Al Merrikh wakati ubao ukisoma Simba 3-0 Al Merrikh.

Gomes amesema kuwa anafurahi uwepo wa nyota wake kwenye mazoezi ambao ni pamoja na Mugalu, Morrison kwa kuwa wamekuwa kwenye ubora wakishirikiana na wachezaji wengine huku wakiwasubiri wengine ambao walikuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa.

“Wachezaji wamekuwa wakifanya vizuri na kila siku wamekuwa wakifanya kazi kubwa jambo ambalo ni jema na uwepo wao kwangu ni furaha,” .

SOMA NA HII  AHAMED ALLY AWEKA WAZI KILICHOMPELEKA GAMONDI KWENYE MECHI YA SIMBA JANA