Home Uncategorized KAHATA NA SIMBA MAMBO YAMEIVA

KAHATA NA SIMBA MAMBO YAMEIVA


Inaweza ikawa taarifa nzuri zaidi kwa mashabiki na wapenzi wa klabu ya Simba ambapo taarifa zinasema mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara bado wapo kwenye mazungumzo na Francis Kahata kwa ajili ya kujiunga nao.

Kahata ambaye amemaliza mkataba na Gor Mahia FC ya Kenya, anaelezwa kufikia pazuri kimazungumzo na Simba na kuna uwezekano mkubwa akajiunga nao mwezi ujao.

Taarifa kutoka Kenya zimeripotiwa kuwa Simba wameendelea kuzungumza na wakala wa mchezaji wake ili kupata saini yake na kuwa uwezekano akasaini mkataba wa miaka miwili.

Kahata hivi sasa yupo na timu yake ya taifa la Kenya huko Misri ambapo michuano ya AFCON inazidi kushika kasi hivi sasa.

Tetesi za mchezaji huyo ambaye ni kiungo fundi zimeanza muda mrefu na uwezekano mkubwa wa kutua Tanzania ipo kwa siku za usoni.

SOMA NA HII  JUVENTUS, REAL MADRID WAPIGANA VIKUMBO KUINASA SAINI YA POGBA