Home Uncategorized MRITHI WA SARRI NDANI YA CHELSE, LAMPARD KUTANGAZWA BAADA YA MASAA 48

MRITHI WA SARRI NDANI YA CHELSE, LAMPARD KUTANGAZWA BAADA YA MASAA 48


Frank Lampard anapewa nafasi kubwa ya kurejea kwenye timu yake ya zamani ya Chelsea akiwa ni meneja ndani ya siku mbili.


Mchezaji huyo wa zamani anatajwa kurejea ndani ya Stamford Bridge pamoja na mchezaji mwingine wa zamani Jody Morrris huku wakitarajiwa kutangazwa ndani ya masaa 48 yanayofuata kwa mujibu wa talkSport.
Lampard mwenye miaka 41 amekuwa akitajwa kuwa chaguo namba moja na Chelsea baada ya meneja aliyepita Maurizio Sarri kusepa ndani ya kikosi hicho na kutimkia Juventus inayoshiriki Serie A wakiwa ni mabingwa.

Lampard anatajwa kumrithi Sarri ambaye licha ya kutwaa ubingwa wa Europa League na kushika nafasi ya tatu kwenye Premier League imeelezwa kwamba alishindwa kuunganisha timu pamoja na mashabiki kutokana na mbinu zake kutopendwa.

SOMA NA HII  KAZE ANA KAZI YA KUPAMBANA NA VIGONGO VITANO VYA MOTO NOVEMBA