Home Uncategorized HILI SASA NI BALAA, MAMA TANASHA AZUIA NDOA YA MONDI NA MWANAYE

HILI SASA NI BALAA, MAMA TANASHA AZUIA NDOA YA MONDI NA MWANAYE


Achana na sababu alizowahi kuzitoa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ juu ya kuahirisha ndoa yake na Tanasha Donna Oketch, lakini kumbe nyuma ya pazia, mama mzazi wa mrembo huyo, Diana Oketch anadaiwa kuwa ndiye chanzo kikuu, Gazeti la Ijumaa limedokezwa.

Diana, mama anayeonekana bado anaita na akitembea na Tanasha unaweza kubisha kuwa siyo mama na mwanaye kutokana na mwonekano wao, anatajwa kuzuia ndoa hiyo ya bintiye na Diamond au Mondi kwa sababu za msingi. Ndoa ya Diamond ambaye ni staa mkubwa wa Bongo Fleva na mrembo huyo mwenye uraia wa Kenya ilikuwa ifungwe Februari 14, mwaka huu (Valentine’s Day) kabla ya kutangazwa kuahirishwa hadi itakapotajwa tena.

Diamond alisema, waliiahirisha ndoa hiyo kutokana na kuwakosa wageni wake mashuhuri akiwemo rapa mkubwa kutoka Marekani, William Leonard Roberts II ‘Rick Ross’.

TUJIUNGE NA VYANZO

Mapema wiki hii, Gazeti la Ijumaa liliperuzi mitandao mbalimbali ya nchini Kenya ambayo iliainisha kuwa, sababu kubwa ya ndoa hiyo kutofungwa ni shinikizo la bi mkubwa huyo. Ilielezwa kuwa, awali Mondi alivyotangaza ndoa hiyo, mama Tanasha alishtuka, akalazimika kuzungumza na bintiye na kumhoji kama anamfahamu vizuri mkali huyo wa Bongo Fleva? “Mama alishtuka kidogo, akataka kujiridhisha kwa bintiye ili kujua kama wanafahamiana kwa muda mrefu.


USHAURI WENYEWE “Alimshauri ajipe muda kwanza, amjue vizuri Diamond maana haiwezekani aingie kwenye ndoa na mtu kabla hajamjua vizuri, anaweza kujikuta ameingia mkenge mbele ya safari,” vyanzo mbalimbali vilinukuliwa kwenye mitandao hiyo.

TANASHA AKUBALIANA NA MAMA’KE

Baada ya kuelezwa hivyo, Tanasha ambaye anatajwa kumsikiliza zaidi mama yake huyo kuliko mtu mwingine yeyote, alikubaliana naye bila kipingamizi chochote. “Ilibidi azungumze na Mondi, Mondi naye alimuelewa na kwa pamoja wakakubaliana kusogeza mbele tukio hilo kwa kuzingatia pia wakati huo Mondi pia alikuwa amewakosa baadhi ya mastaa wakubwa akiwemo Rick Ross ambao alitamani wawepo kwenye shughuli yake,” chanzo kingine kilinukuliwa.

BI MKUBWA APONGEZWA

Maoni mbalimbali yaliyowekwa kwenye habari hiyo ya mama Tanasha na kusindikiza na picha mbalimbali za mrembo huyo akiwa na mama yake, yalionesha kumpongeza mzazi huyo kwa ushauri huo wa msingi kwani hakutaka mwanaye aonekane anakurupuka.

Waliutaja ushauri huo kwamba ni wa busara na kwamba pindi watakapokaa kwa muda mrefu kidogo, watakuwa wamesomana na kujuana tabia vya kutosha. “Raha ya uhusiano ni mtu kumjua angalau kidogo mwenza wake, siyo tu ghafla mnatangaziana ndoa, hiyo siyo sawa kwa kweli,” alichangia mdau mmoja aliyejiita Kinya mtandaoni.

TANASHA AKATA MZIZI WA FITINA

Baada ya vyanzo hivyo kumwaga data hizo, juzi, Tanasha mwenyewe alikata mzizi wa fitina baada ya kuufungukia Mtandao wa Kiss100 wa nchini Kenya sababu zilizomfanya aahirishe kuingia kwenye ndoa haraka.

Hata hivyo, sababu hizo hazikutofautiana na zile zilizosemekana kutajwa na mama yake. Alianza kwa kusema alifanya hivyo kwa sababu alitaka kwanza kuiandaa familia yake kulipokea tukio hilo zito maishani mwake. Lakini zaidi alisema kuwa, walikubaliana waiahirishe ndoa hiyo ili pia waweze kujuana kiundani na Diamond kabla ya kuwaeleza wazazi wake na familia yake kwa jumla.

“To be honest, we decided to take our time and focus on getting to know each other; loving each other…And definitely, wedding plans will come God-willing,” alinukuliwa Tanasha kwa kimombo. Katika tafsiri isiyo rasmi akiwa na maana; “Kiukweli tulikubaliana kujipa muda na kuweza kujuana zaidi, kupendana zaidi na moja kwa moja ndoa itajileta yenyewe kwa mapenzi ya Mungu.”

TANASHA NA MONDI

Penzi la Tanasha na Mondi liliibuka mwishoni mwa mwaka jana ambapo Wabongo waliweza kuwaona kwa ukaribu zaidi wawili hao katika Tamasha la Wasafi Festival lililozunguka katika baadhi ya mikoa nchini. Hata hivyo, miezi kadhaa ya penzi lao bila ndoa, tayari Mondi anadaiwa ‘kumharibu’ Tanasha kwa kumpachika mimba ambayo inatajwa kuwa ni kubwa kwa sasa.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YATOSHANA NGUVU NA YANGA JAMHURI, MOROGORO