Home Yanga SC MRUNDI WA YANGA APEWA PROGRAM MAALUMU

MRUNDI WA YANGA APEWA PROGRAM MAALUMU


 KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, ameanza mazoezi katika timu hiyo kwa program maalum kabla ya kuungana na wenzake katika mazoezi ya pamoja.

Hiyo ikiwa ni siku moja tangu kiungo huyo atue nchini akitokea kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Burundi ikitoka kucheza michezo ya kuwania kufuzu AFCON.

 

Staa huyo amekosekana ndani ya kikosi cha Yanga kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na kuuguza maumivu ya nyonga.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema kiungo huyo alijiunga na kambi hiyo Jumamosi iliyopita akitokea kwao Burundi.

 

Saleh alisema mara baada ya Saido kutua, haraka alianza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kuungana na wenzake kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC.

 

Aliongeza kuwa timu hiyo inaendelea vizuri katika kuelekea mchezo huo dhidi ya KMC, morali ya wachezaji ni kubwa katika kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye ligi.

 

“Timu inaendelea vizuri na maandalizi kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya KMC, Saido tayari yupo kambini na ameanza mazoezi kwa program maalum chini ya Kocha Mwambusi (Juma).

 

“Kurejea kwa Saido kutaimarisha kikosi chetu kuhakikisha timu inapata ushindi katika michezo ijayo ya ligi ili tuendelee kukaa kileleni,” alisema Saleh.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA BRUNO KUTUA YANGA...UKWELI WA MAMBO UKO HIVI....JAMBO LILIISHA MAPEMA TU...