Home Yanga SC MWAMBUSI: HAIKUWA MPANGO WETU KUPATA SARE

MWAMBUSI: HAIKUWA MPANGO WETU KUPATA SARE

JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga amesema kuwa sare waliyopata jana haikuwa kwenye mpango wao ila kwa kuwa wamepata pointi moja basi ni jambo la kushukuru.

Ikiwa Uwanja wa Mkapa, jana Aprili 10 ilikwenda mapumziko huku ubao ukisoma Yanga 0-1 KMC na mtupiaji wa KMC alikuwa ni David Bryson dakika ya 28. 

Kipindi cha pili Yanga walianza kwa kasi na kutupia bao la kuweka usawa dakika ya 46 kupitia kwa Yacouba Songne. 

Sare hiyo inaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 51 ikiwa nafasi ya kwanza huku KMC ikifikisha pointi 36 na ipo nafasi ya sita.

Mwambusi amesema kuwa hawakupanga kupata pointi moja kutokana na maandalizi ambayo walikuwa wameyafanya.

“Hatukupanga kupata pointi moja ila kwa kuwa siku zote nimekuwa nikisema tangu awali kuwa KMC huwa inakuwa bora ikikutana na Yanga na hata ukitazama nafasi yake bado inaonyesha ni timu yenye ushindani.

“Makosa ambayo yamejitokeza tunayafanyia kazi kwa ajili ya mechi zetu zijazo. Ninawapongeza wachezaji wangu kwa kuwa walipambana na bado hatujakata tamaa,” .

SOMA NA HII  KISA DJUMA KUSIMAMISHWA..YANGA WALIA UHABA WA MABEKI...BACCA ATAJWA KUSIMAMIA SHOW ZIJAZO...