Home Ligi Kuu KUMBE COASTAL UNION WALICHEZA KWENYE BWAWA WAKATI WAKIKUBALI KICHAPO CHA 4G

KUMBE COASTAL UNION WALICHEZA KWENYE BWAWA WAKATI WAKIKUBALI KICHAPO CHA 4G

 

BAADA ya kupoteza kwa kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Gwambina FC, jana Aprili 10, Uwanja wa Gwambina Complex, Wagosi wa Kaya wamesema kuwa uwanja waliochezea haukuwa rafiki kwao kwa kuwa ulikuwa na maji kama bwawa.

Gwambina walianza kupachika  bao la kwanza dakika ya 9 kupitia kwa Meshack Abraham, Paul Nonga akaongeza la pili dakika ya 31 na msumari wa tatu ulipachikwa na Rajab dakika ya 37.

Mpaka muda wa mapumziko ubao wa Gwambina Complex ulikuwa unasoma Gwambina FC 3-0 Coastal Union.

Vijana hao wa Coastal Union wanaonolewa na Juma Mgunda kipindi cha pili waliokota nyavuni bao dakika ya 75 lilipachikwa kimiani kupitia kwa Jimson Mwanuke.

Kupitia ukurasa rasmi wa  Instagram wa CoastalUnion wamesema kuwa wameshindwa kupata matokeo kwa kuwa walicheza kwenye bwawa la Gwambina, mjini Mwanza.

Kwenye msimamo Coastal Union ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 27 na Gwambina FC ipo nafasi ya 10 ina pointi 30.

SOMA NA HII  JINSI USHINDI WA SIMBA SC DHIDI YA POLISI TZ ULIVYOISAIDIA YANGA LEO...