Home Yanga SC NENO LA NCHIMBI BAADA YA KUFUNGA BAO MBELE YA GWAMBINA

NENO LA NCHIMBI BAADA YA KUFUNGA BAO MBELE YA GWAMBINA


 MSHAMBULIAJI mzawa ndani ya Klabu ya Yanga, Ditram Nchimbi amesema kuwa hakumbuki mara ya mwisho kufunga ilikuwa lini katika mechi zake za ushindani.

Nyota huyo alipitisha mwaka mzima bila kufunga kwenye mechi za ushindani ila aliweza kufunga jana Aprili 20 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC.

Kwenye mchezo huo Yanga ilishinda mabao 3-1 kisha ilisepa na pointi tatu jumlajumla. Mabao mengine yalifungwa na Bakari Mwamnyeto na Saido Ntibanzokiza ambaye alipofunga aliomba kufanyiwa mabadiliko na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi.

Bao la Gwambina FC lilifungwa na Jimsone Mwanuke ambaye alipachika bao hilo akiwa nje ya 18 likamshinda mlinda mlango, Faroukh Shikalo.

Nchimbi amesema:”Mara ya mwisho sikumbuki ilikuwa lini nimefunga ila nimefurahi kuona kwamba nimefunga kwa kuwa ushindi ni jambo la msingi na tumefurahi,” amesema.

Yanga ikiwa imefunga mabao 41 yeye ametupia bao moja na ametoa pasi mbili za bao.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU 2022/23 ...HAWA HAPA JUMLA YA MASTAA WOTE WA YANGA WATAKAO PEPERUSHA BENDERA YA NJANO NA KIJANI...