Home Uncategorized KAZI IMEANZA SIMBA WAJIBU MAPIGO YA YANGA, WAANZA NA BOCCO MIAKA MIWILI

KAZI IMEANZA SIMBA WAJIBU MAPIGO YA YANGA, WAANZA NA BOCCO MIAKA MIWILI

UNAAMBIWA Uongozi wa Simba baada ya kuona watani zao wa jadi Yanga wao wameanza na kiungo fundi Papy Tshishimbi kumuongezea mkataba wao wameanza kujibu kwa kuanza na nahodha wa kikosi hicho John Bocco.

Bocco ni miongoni mwa nyota wanne ambao wamejiunga na kikosi hicho wakitokea Azam FC akiwa pamoja na mlinda mlango Aishi Manula, beki kiraka Erasto Nyoni, Shomari Kapombe ambao nao imeelezwa wameshamalizana na Simba.

Kupitia ukurasa wa Istagram wa Simba umeeleza kuwa nahodha wao John Bocco amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea klabu yetu. 

Bocco alikuwa mchezaji bora wa Simba na Ligi Kuu kwa msimu wa 2017/18 na Mshambuliaji Bora kwa msimu wa 2018/19 amefunga jumla ya mabao 30 ya Ligi katika misimu miwili.

SOMA NA HII  SURE BOY WA AZAM FC RUKSA KUIBUKIA YANGA