Home Simba SC SIMBA WAANZA KUTOA SABABU KABLA YA KUVAANA NA GWAMBINA LEO

SIMBA WAANZA KUTOA SABABU KABLA YA KUVAANA NA GWAMBINA LEO




 IKIWA leo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes inatarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya Gwambina FC imeweka wazi kwamba Uwanja wa Gwambina Complex sio rafiki kwao.

Sababu hii pia ilitajwa wakati wakipata ushindi kwa tabu mbele ya Mwadui FC baada ya ubao kusoma Mwadui 0-1 Simba bao lililopachikwa na John Bocco dakika ya 66.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanatambua utakuwa mchezo mgumu ila sehemu ambayo wanachezea sio rafiki.

“Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Gwambina ila tunatambua kwamba hautakuwa mchezo mwepesi hilo lipo wazi lakini uwanja kwetu sio rafiki.

“Tutajitajihidi kufanya vizuri tumeona sehemu ya kuchezea sio nzuri lakini hakuna namna ni lazima tupambane ili kupata matokeo chanya,” amesema.

Kwenye msimamo wa ligi, Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 55 baada ya kucheza mechi 23 inakutana na Gwambina FC iliyo nafasi ya 12 na pointi 30.

 

SOMA NA HII  UMAFIA, SIMBA WAICHAMBUA YANGA KWA MTINDO HUU, WATAJA MAKOSA YAO