Home Habari za michezo WAKATI YANGA WAKIJITAFUTA …..SIMBA YAZIDI KUTAKATA CAF…WAIPITA TP MAZEMBE KWA KILA KITU…

WAKATI YANGA WAKIJITAFUTA …..SIMBA YAZIDI KUTAKATA CAF…WAIPITA TP MAZEMBE KWA KILA KITU…

Habari za Simba

IFFHS imetoa orodha ya timu 10 bora za mwezi za CAF ambapo zimeionyesha Simba ya Tanzania kuwa ni ya 9 kwa ubora katika klabu zote za Afrika.

Simba ambayo ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa, wakiwa katika nafasi ya pili kwenye kundi C mbele ya Raja Casablanca , imekamata nafasi hiyo ikiwa na alama 113.

Raja Casablanca ambao ni wapinzani wa Simba kwenye kundi C, wao wako nafasi ya 8 wakiwa na point 117.

Kwenye viwango hivyo vya ubora bado Al Ahly wanashika nafasi ya kwanza wakiwa na alama 220, wakifuatiwa na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo wao wanapoint 170.

Kwenye orodha hiyo, hakuna timu nyingine kutoka ukanda wa CECAFA zaidi ya Al Hilal yenye pointi 132.75 kisha inafuatiwa na Simba yenye alama 113 nafasi ya 9.

Yanga pamoja na kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kombe la shirikisho, yenyewe bado haijaweza kupenya kuingia hata kwenye 10 bora, huku TP Mazembe wakishuka mpaka kwenye 20 bora ya msimamo huo.

1. Ahly – 220 points
2. Wydad – 170 points
3. Zamalek – 154 points
4. Pyramids- 140.5 points
5. Al Hilal – 132.75 points
6. Mamelodi- 127 points
7. CR Belouzidad – 117.75 points
8. Raja Casablanca – 117 points
9. Simba SC – 113 points
10. Petro Luanda – 112 points

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI