Home Yanga SC TFF YAMJIBU MWAKALEBELA KUHUSU HUKUMU YAKE YA MIAKA MITANO

TFF YAMJIBU MWAKALEBELA KUHUSU HUKUMU YAKE YA MIAKA MITANO


 SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) limefafanua kuwa adhabu aliyopewa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kuwa imeegemea kwenye upande wake wa uongozi wa klabu na si kwenye masuala mengine ya kama vile kumzuia asifuatilie taarifa za michezo.

 

 Ndimbo amejibia malalamiko ya Makamu Mwenyekiti huyo aliyefungiwa kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 5 na faini ya shilingi milioni 7 kuwa, siku tatu zilizopita alisema amezuiwa asisome magazeti ya michezo wala kutazama runinga.

 

 Ndimbo amesema;- “Kama ambavyo taarifa ya adhabu ilivyosema na ni tofauti na alivyoielezea kwamba haruhusiwi hata kusoma magazeti au ikifika kwenye taarifa za michezo azime TV asiangalie. 


“Adhabu aliyopewa ni kwamba majukumu yake ambayo amekuwa nayo ndipo aadhabu ilipoegemea.

 

 

“Asijihusishe na majukumu hayo ya kiuongozi kwa muda huo ila mengine kuhusu kutokusoma magazeti labda alikuwa anafurahisha genge tu.”

 

 

(Aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela ambaye kwa sasa amefungiwa miaka 5).

 

 

Ndimbo amesema Mwakalebela amefungiwa kimajukumu ya Uongozi lakini ana nafasi ya kushuhudia michezo viwanjani kama mashabiki wengine.

 

 

“Linapokuja suala la kwenda uwanjani hilo sio kujishugulisha na suala la uongozi wa mpira na maana yake umekwenda kama mtazamaji mwingine.”


SOMA NA HII  YANGA HII YA GAMONDI SIO POA CHEKI BALAA LAKE