Home news BREAKING: MSIMU UJAO KAHATA KUVAA JEZI ZA KIJANI..MCHONGO MZIMA UKO HIVI

BREAKING: MSIMU UJAO KAHATA KUVAA JEZI ZA KIJANI..MCHONGO MZIMA UKO HIVI


Klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya ambayo hutumia jezi za kijani kwenye mechi za nyumbani
 imepanga kumrudisha kiungo wao wa zamani, Francis Kahata, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa miaka miwili na Klabu ya Simba kuisha.

Kahata anaweza kujiunga na Klabu hiyo ya kwao Kenya, licha ya kuhusishwa na Vilabu mbalimbali kutoka Sudani, Afrika Kusini na Zambia.

Taarifa kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa, kiungo huyo ana nafasi kubwa ya kurudi Gor Mahia , kufuatia ushawishi kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo, pamoja na watu wake wa karibu.

Hata hivyo Kahata hajasema lolote mpaka sasa, licha ya kufahamika ana ofa zaidi ya moja mkononi mwake katika kipindi hiki cha dirisha la usajili.

Kahata aliitumikia Simba SC kwa mafanikio makubwa ndani ya misimu miwili, akichangia upatikanaji wa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho kwa mara mbili mfululizo.

SOMA NA HII  EDO KUMWEMBE:- SIMBA INAWEZA ISIPITE ....KIBU DENIS SIO MIQUISSONE...HAWANA IMANI NA BOCCO...