Home Yanga SC YANGA KAMILI GADO KWA AJILI YA MECHI ZA LIGI KUU BARA NA...

YANGA KAMILI GADO KWA AJILI YA MECHI ZA LIGI KUU BARA NA SHIRIKISHO


 JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga amesema kuwa maandalizi ya vijana wake yapo vizuri jambo ambalo linampa furaha ya kufanya vizuri kwenye mechi zake zijazo.

Kikosi hicho kipo kambini Kigamboni kikiendelea na maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara ni dhidi ya KMC ambao unatarajiwa kuchezwa Aprili 10, Uwanja wa Mkapa.

Walipokutana Uwanja wa CCM Kirumba, ubao ulisoma KMC 1-2 Yanga, ilikuwa zama za Cedric Kaze ambaye alichimbishwa Machi 7 kwa kile ambacho kilielezwa kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo.

Mwambusi amesema:-“Wachezaji wanazidi kuimarika na wapo tayari kwa ajili ya mechi zijazo, hata katika mazoezi wanaonekana kuwa imara jambo ambalo ni jema.

“Kikubwa ambacho ninaamini watafanya ni kuleta utofauti na kupata matokeo kwenye mechi zijazo kwani kila kitu kinakwenda sawa,” ,

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.

Inafuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili na ina pointi 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 20.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTWAA UBINGWA LIGI KUU....YANGA WAOMBWA KWENDA BUNGENI...SPIKA DK TULIA 'AWACHEULIA NNJE'...