Home Yanga SC YANGA: TUTAFANYA VIZURI NAFASI IPO

YANGA: TUTAFANYA VIZURI NAFASI IPO

 


JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa bado kuna nafasi ya kikosi chake kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara.

Aprili 10 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-1 KMC katika mchezo wa ligi ikiwa ni mzunguko wa pili.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa CCM Kirumba, ubao ulisoma KMC 1-2 Yanga na kuwafanya vinara hao wa ligi kuvuna jumla ya pounti nne kati ya sita mbele ya Wanakino Boys.

Mwambusi amesema kuwa ana matumaini na wachezaji wake kuelekea mechi zijazo watapambana na kupata matokeo.

“Kupata pointi moja mbele ya KMC sio jambo baya tunashukuru kwa kuwa tulikuwa tunahitaji pointi tatu, ila kwa kuwa kuna mechi nyingine nina amini tutafanya vizuri. 

“Kama ambavyo nilikuwa nikisema kwamba KMC huwa inakuwa bora kila inapokutana na Yanga hicho tumeshuhudia na tumeona, kikubwa ni kujipanga upya kwani ligi bado inaendelea,” .

Kwenye msimamo wa ligi Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 24 KMC ipo nafasi ya 6 na pointi 36 baada ya kucheza mechi 25.


SOMA NA HII  YANGA YAWEKA REKODI HII YA KIPEKEE LIGI KUU