Kocha Mkuu, Didier Gomez na wasaidizi wake wamepanga kikosi kamili kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya 16 bora dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa leo saa moja usiku.
Gomez amewaanzisha mlinda mlango namba moja Aishi Manula akisaidiwa na walinzi Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Joash Onyango na Pascal Wawa.
Katika eneo la kiungo wa ukabaji amewaanzisha Taddeo Lwanga na Jonas Mkude huku washambuliaju wakiwa ni Clatous Chama, Luis Miquissone na Rally Bwalya wakati idara ya ushambuliaji itaongozwa na Medie Kagere.
Baadhi ya wachezaji wanaoanzia benchi ni washambuliaji John Bocco, Chris Mugalu na kiungo mshambuliaji Bernard Morrison.
Kikosi Kamili kilichopangwa
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohamed Hussein Β©
4. Joash Onyango
5. Pascal Wawa
6. Taddeo Lwanga
7. Clatous Chama
8. Jonas Mkude
9. Medie Kagere
10. Rally Bwalya
11. Luis Miquissone
Wachezaji wa Akiba
Gk. Beno Kakolanya
02. David Kameta
03. Erasto Nyoni
04. Mzamiru Yassin
05. Chris Mugalu
06. John Bocco
07. Bernard Morrison