SHABIKI wa Simba, maarufu kama Simba Ulaya amesema kuwa mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Kagera Sugar wakati wakishinda mabao 2-1 ulikuwa ni mpango wa timu hiyo kupanga kikosi kitakachoanza kwenye mchezo dhidi ya Yanga, Mei 8.
Ameongeza kuwa wanaweza kupata penalti tano kwenye mchezo huo ambao unazidi kuwa na joto kwa sasa.