Home kimataifa NYOTA VIDAL NOMA, ATWAA MATAJI 9 NDANI YA MIAKA 10

NYOTA VIDAL NOMA, ATWAA MATAJI 9 NDANI YA MIAKA 10


 BAADA ya kutwaa taji la ubingwa wa Serie A msimu huu kiungo Inter Milan, Arturo Vidal amefanikiwa kutwaa mataji tisa ya ligi tofauti ndani ya miaka 10.

Vidal amefanikiwa kutwaa mataji hayo akiwa na Juventus ambapo alishinda manne ya Serie A, 2012 mpaka 2015.

Ndani ya Bundesliga na kikosi cha Bayern Munich alibeba taji la ligi hiyo mara tatu msimu wa 2015/16, 2016/17 na 2017/18.

Msimu wa 2018/19 alitwaa taji la La Liga akiwa na Barcelona ambapo aliondoka msimu uliopita na kutua Inter Milan.

Katika miaka hiyo 10 Vidal hakushinda taji msimu wa 2019/0 akiwa ndani ya Barcelona na ni msimu pekee ambazo hakutoka na taji la ligi.

SOMA NA HII  UEFA YAMPANGA REFA MWENYE BAHATI NA MADRID KUCHEZESHA FAINAL YA LIVERPOOL vs MADRID...