epl

CHELSEA YATINGA FAINALI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

admin May 6, 2021 2:47 am


UWANJA wa Stamford Bridge, usiku wa kuamkia leo, Chelsea inayonolewa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel imefungua njia na kutinga hatua ya fainali ya UEFA Champions League. 

Mabao 2-0 dhidi ya Real Madrid yanawafanya watinge fainali kwa jumla ya mabao 3-1 mbele ya Kocha Mkuu wa Real Madrid, Zinedine Zidane ambaye alikwama kuibuka na ushindi.

Ni Timo Werner alifunga bao la ufunguzi dakika ya 28 na Mason Mount alipachika bao la pili dakika ya 85 huku lango la Chelsea likiwa katika mikono salama ya Eduardo Mendy.

Ushindi huo unaipa tiketi Chelsea kukutana na Manchester City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola katika fainali inayotarajiwa kuchezwa Mei 29.

Kabla ya kucheza fainali ya UEFA itaanza kazi ya kusaka taji la FA Mei 19 mbele ya Leicester City, Uwanja wa Wembley.


HUYU HAPA KIPA WA YANGA REKODI ZINAMBEBA MBELE YA SIMBA KUMBE! SIMBA WANAAMINI KWAMBA TAREHE 8 HAWATOKI MBELE YA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply