MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga uliotarajiwa kuchezwa leo Mei 8 umeahirishwa.
Sababu kubwa ya mchezo wa leo kuahirishwa ni kutokana na mabadiliko ya muda wa awali ambao ulipangwa kuwa saa 11:00 jioni ila ghafla Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) likatuma taarifa ya kubadili muda mpaka saa 1:00 usiku.
Kwa mujibu wa Yanga wameeleza kuwa hawawezi kucheza mchezo huo kwa kuwa TFF imekiuka kanuni ya kubadili muda kanuni ya 15, (10) za Ligi Kuu Bara ambayo inaeeleza kuwa;”Mabadiliko yoypte ya muda wa kuanza mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote husika za mchezo angalau saa 24 kabla ya muda wa awali,”.
Yanga ilipeleka kikosi uwanjani saa 11: 00 na wachezaji walifanya warm up kisha Simba walifuata baadaye.