Home Habari za Simba Leo SERGE POKOU ANASA SIMBA…KILA KITU TAYARI

SERGE POKOU ANASA SIMBA…KILA KITU TAYARI

0
Habari za Simba leo- Serge Pokou

HABARI ZA SIMBA LEO, Inaaminikaa kwamba klabu hiyo wiki hii imepanga kumsaini kiungo wa Asec Mimosas, Serge Pokou kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh200mil.

Siku za hivi karibuni iliripoti kuwa Simba imekuwa ikimfuatilia kwa ukaribu zaidi kiungo ( Serge N´guessan Archange Pokou), ambaye ni panga pangua wa Asec Mimosas, na wamekubaliana sehemu kubwa ya dili hilo, ili mwamba huyo aje kukipiga kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Ni kijana mdogo aliyezaliwa mwaka 2000, na sasa ana umri wa miaka 23, makuzi yake kwa kiasi kikubwa ni kucheza mpira akianzia safari yake kwenye klabu ya Moossou Football Club, ya nchini kwao Ivory Coast, lakini alijiunga na Asec Mimosas na kudumu kwa misimu minne yenye mafanikio makubwa.

Serge Pokou ni sehemu ya kikosi cha Asec kilichocheza na Mnyama Simba kwenye Ligi ya Mabingwa msimu uliomalizika, na hadi sasa kiungo huyo amecheeza mechi 12, amefunga mabao 3 na kutoa pasi 1 ya goli.

Ikumbukwee pia nyota huyu amekuwa akifuatiliwa kwa ukaribu zaidi na Yanga na vilabu vingine vya Afrika, lakini Simba ndiyo wapo kwenye nafasi kubwa zaidi ya kuinasa saini ya Serge Pokou tena kwa dau dogo kabisa la Tsh Milioni 200/=

Simba inapambana kukisuka vizuri kikosi chake ambacho kwa msimu uliomalizika 2023.24 kwa miaka ya hivi karibuni kimekuwa sio tishio sana, hivyo Mabosi wa klabu hiyo wapo makini sana kwenye kufanya sajili ili kuendana na mahitaji yao, tena kwa kuzingatia umri.

Tayari maboresho yameshafanyika ndani ya Uongozi wa Simba haswa upande wa kamati ya usajili, vichwa kadhaa vimeongezwa ili kusimamia suala hilo, kuna Magori, Sued Nkwabi, Mulamu, na Kassim Dewji hawa jamaa wanatoka kwenye kundi la “Friends of Simba” ambalo lilikuwa msaada mkubwa sana kwa mafanikio ya Simba kwa misimu mingi.