Home Simba SC SIMBA: TUMESHANGAZWA NA KILICHOTOKEA, TULIJIAANDAA KUCHEZA

SIMBA: TUMESHANGAZWA NA KILICHOTOKEA, TULIJIAANDAA KUCHEZA


BAADA ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba v Yanga kughairishwa leo Mei, 8, uongozi wa timu hiyo umesema kuwa ulikuwa unajiamini na ulijiandaa kwa ajili ya mchezo wa leo.


Ni Yanga waliamua kuondoka uwanjani kutokana na ratiba ya muda kupelekwa mbele ghafla ambapo awali ilikuwa uchezwa saa 11:00 jioni na ukapelekwa mbele mpaka saa 1:00 usiku.


Didier Gomes,  Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa walijipanga kwa ajili ya mchezo wa leo ila wameshtushwa na kilichotokea kwa kuwa wote walipokea taarifa muda mmoja. 


“Hamna namna kwetu imekuwa ni mshtuko kwa kilichotokea, tulijandaa na tulikuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.


“Zaidi ni kwamba tunaweza kusema kwamba kwa mashabiki ambao walijitokeza kuona burudani haijawa hivyo tunarudi kambini kwa ajili ya maandalizi mengine kwani tunatarajia kuondoka Jumatatu,”.

Kikosi cha Simba kiliwasili uwanjani nankupishana na wachezaji wa Yanga ambao waliingia uwanjani saa 10 na kufanya mazoezi kwa ajili ya kukiaanda kikosi chao na muda waliokuwa wanautambua ni ule wa saa 11:00. 


Simba inatarajiwa kukwea pipa Jumatatu kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs.

SOMA NA HII  VIDEO: HATARI YA KAIZER CHIEFS MBELE YA SIMBA ZATAJWA,