Simba SC

SIMBA: TUMECHEZA HOVYO, TUMEADHIBIWA

admin May 16, 2021 4:47 am


BAADA ya dakika 90 kukamilika na ubao wa Uwanja wa FNB Soccer City kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba, Ofisa Habari wa Simba,  Haji Manara amesema kuwa walicheza hovyo.

Kichapo hicho kinakuwa cha kwanza kwa Kocha Mkuu Didier Gomes kushuhudia idadi kubwa ya mabao kwa timu yake ikifungwa akiwa katika benchi baada ya kupokea mikoba ya Sven Vandenbroeck.

Haji Manara kupitia Ukurasa wake wa Istagram alisema:” Alhamdulillah. Tumefungwa na aliye bora usiku wa leo, tumecheza hovyo na tumefanya makosa mengi yaliyostahili adhabu hii.

“Life go on, (maisha lazima yaendelee) na still, (bado) tunazo dk tisini nyingine za kuamua,”.

Mchezo wa robo fainali ya pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22 ambapo Simba wanapaswa kufunga mabao zaidi ya manne ili kusona mbele hatua ya nusu fainali.


MRUNDI WA YANGA HATAMANI KUBAKI KIKOSINI HAPO LEICESTER CITY YASEPA NA TAJI LA KWANZA LA FA MBELE YA CHELSEA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply